Kuhusu FADEMO
Tunajenga familia imara za kiuchumi kupitia maarifa, hifadhi ya jamii na miradi chanya ya maendeleo.
FADEMO ni kifupisho cha Family Development Motivators, jina linalotumika kwenye shughuli zote za biashara na huduma zinazoratibiwa na FADEMO na makampuni yake tanzu.
Kuwa Kampuni kubwa Tanzania inayotoa huduma bora za kujenga Familia zenye uchumi imara na hatimaye Taifa lenye uchumi imara.
Kutoa taarifa na maarifa ya elimu ya kifedha, uchumi na maendeleo; kusimamia Mfuko wa Jamii unaotoa mafao bora; pamoja na elimu ya afya, mazingira na masuala ya kijamii.
- Kuweka mbele Maslahi ya Wateja (Customer Focus)
- Uadilifu (Integrity)
- Weledi Mkubwa (Professionalism)
- Uaminifu (Trustworthy)
- Ushirikiano na Jamii (Social Unity)
- Mshikamano (Solidarity)
- Uwazi (Transparency)
- Mfuko wa Jamii wa FADEMO (FADEMO Social Fund Trust Tanzania)
- FADEMO School of Blockchain Ltd
- FADEMO Books Publishing Ltd
- FADEMO Blogs & News (Fademo Newsmedia)
- FADEMO Online Television Ltd
- FADEMO Building & Constructions Ltd
- FADEMO Electrical Installations Ltd
- Miradi: “Mchwa ni Adui wa Nyumba”, “Familia ni Afya Imara”
Mfuko huu unalenga kuwawezesha wanachama wake kukabiliana na majanga pamoja na changamoto za kiuchumi zinazowakabili wajasiriamali wengi kwa sababu uzee, magonjwa magonjwa makubwa, vifo vya wakuu wa familia, majanga ya asili majanga ya kiuchumi na kijamii ambayo huweza kuepukwa kama tu kuna mfumo rasmi wa kuwakinga na majanga hayo.
Lengo kuu la Mfuko wa Jamii wa FADEMOKutoa mafao makubwa ya kukabiliana na majanga ya kijamii na kiuchumi wanachama kwa wajasiriamali wote ambao hawana Mfumo rasmi wa Hifadhi ya Jamii unaowakinga na majanga ya kiuchumi.
Mafao ya Muda Mrefu
- Kiinua Mgongo
- Pensheni Uzeeni
- Watoto Yatima
- Pensheni ya Mjane
- Kusomesha Mtoto Shule
Mafao ya Muda Mfupi
- Uzazi
- Matibabu
- Msaada wa Mazishi
- Msiba Nyumbani Kwako
- Msaada wa Ujenzi wa Nyumba
- Majanga (moto, mafuriko, tetemeko)
- Kujitoa (Withdrawal Benefits)
Ofisi
Mtaa wa Ujiji/Tabora, Jijini Dodoma (Kata ya Viwandani),
Katika Jengo la Mkamba Uhindini.
Mkurugenzi Mtendaji
FADEMO GROUP LIMITED,
S.L.P. 49, DODOMA
Simu
0762 812 271 · 0678 207 631 · 0762 170 509
Barua Pepe
Tovuti & Mitandao
Facebook / Instagram / TikTok: (inapatikana)